Beijing. Makubaliano ya mgao wa nguo yafikiwa.
6 Septemba 2005Umoja wa Ulaya na China zimefikia makubaliano kuruhusu mamilioni ya nguo kutoka China zilizozuiliwa na maafisa wa forodha wa umoja huo kwa sababu zimekiuka mgao wa uingizaji nguo hizo.
Kamishna wa biashara wa Umoja wa Ulaya Peter Mandelson amesema kuwa chini ya makubaliano hayo pande zote mbili zitagawana mzigo wa ziada wa mauzo hayo mwaka huu, huku China ikikubali kupunguza uingizwaji wa nguo hizo mwaka ujao katika mataifa ya umoja wa Ulaya.
Makubaliano hayo yanaingiliana na mwanzo wa kikao cha pamoja kati ya umoja wa Ulaya na China kinachokusudia kuimarisha mahusiano ya kibiashara na kupambana na tatizo la hali ya ujoto duniani.
Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair , ambaye ni rais wa sasa wa umoja wa Ulaya , amesema ushirika wa kimbinu kati ya China na umoja huo ni muhimu.