Beijing. Mafuriko yauwa 64 nchini China.
11 Juni 2005Matangazo
Watu 64 wengi wao wakiwa watoto wamekufa katika mafuriko yaliyoharibu shule ya msingi kaskazini mashariki ya China.
Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kuwa waokoaji bado wanawatafuta wanafunzi ambao wamechukuliwa na maji katika mafuriko hayo katika mji wa Shalan katika jimbo la Heilongjiang. Eneo kubwa la mji huo bado limejaa maji kiasi cha mita moja.