Beijing. Mafuriko yaua 567 nchini China.
25 Juni 2005Beijing. Mafuriko yaua 567 nchini China.
Mafuriko makubwa nchini China yamewauwa watu 567 na kuwalazimisha wengine zaidi ya milioni mbili kuyahama makaazi yao kwa mujibu wa taarifa kutoka katika vyombo vya habari vya nchi hiyo.
Rais Hu Jintao amewataka maafisa kuongeza misaada kwa raia.
Gharama za uharibifu unaotokana na mafuriko hayo zinakadiriwa kufikia Euro bilioni 1.3. Mafuriko mabaya kabisa kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni yalitokea mwaka 1998, ambapo watu 4,150 walifariki.