BEIJING: Mafuriko yasababisha vifo 91 nchini China
12 Juni 2005Matangazo
Idadi ya vifo vilivyosababishwa na mafuriko katika shule ya msingi ya Shalan,nchini Uchina yaendelea kuongezeka.Hadi watu 91,wengi wao wakiwa watoto wamepoteza maisha yao katika mafuriko ya ghafla yaliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha siku ya Ijumaa.Walimu 30 na wanafunzi wapatao mia kadhaa walikuwepo ndani ya shule ya kijiji cha Shalan,kaskazini-mashariki mwa Uchina.Mpaka hivi sasa kiasi ya watu 400 wamenasa katika shule hiyo.