Beijing. Mafuriko yaleta maafa China.
11 Juni 2005Matangazo
Kiasi cha watoto 36 na watu wazima wawili wamekufa baada ya mafuriko kuharibu shule ya msingi katika eneo la kaskazini mashariki ya China. Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kuwa watu wengine 17 wamepelekwa hospitalini kutokana na mafuriko hayo katika mji wa Shalan katika jimbo la Heilongjiang.
Waokoaji bado wanawatafuta wanafunzi watano na wanakijiji wawili. Karibu mji wote umejaa maji kiasi mita moja.