Beijing: Maendeleo wastani katika mazungumzo ya kinyuklea
28 Februari 2004Matangazo
BEIJING: Yale mazungumzo ya mataifa sita yaliyomalizika mji mkuu wa Uchina yameshindwa kuusuluhisha mvutano kati ya Washington na Pyongyang kuhusu programu ya kinyuklea ya Korea ya Kaskazini. Wawakilishi wa Marekani, Urusi, Japan na Uchina pamoja na nchi mbili za Korea waliwafikiana ifanyike duru nyingine ya mazungumzo mjini Beijing mwezi wa Julai pamoja na kuundwa kundi la washauri litakalofafanua maswali ya ubishi, alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uchina Li Zaoxing. Katika mkutano huo, Korea ya Kaskazini ilisema itayari kuzuiya programu yake ya kinyuklea, lakini iachiliwe kuzalisha nishati ya kinyuklea. Lakini Marekani inadai kuwa nchi hiyo ya kikomunisti ikomeshe kabisa programu yake ya kinyuklea ndipo itakubalia kusaini mkataba wa kutoshambuliana kijeshi.