BEIJING: Maandamano kuipinga Ujapani
10 Aprili 2005Matangazo
Nchini Uchina kumefanywa maandamano mapya dhidi ya Ujapani.Vyombo vya habari nchini humo vimesema waandamanaji kwa maelfu walimiminika barabarani katika miji miwili ya kusini.Mia kadhaa walikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Ujapani mjini Guangzhou,na wengine walijaribu kuuvuka mpaka wa polisi.Katika mji wa jirani wa Shenzhen,kiasi ya waandamanaji 500 walipaza sauti kuipinga Ujapani na walirusha chupa zenye rangi kwenye mikahawa ya Kijapani.Hisia za chuki dhidi ya Ujapani zimeshika kasi tangu serikali ya Tokyo kuidhinisha kitabu cha shule ambacho wakosoaji wanasema kinaficha ukatili uliotendwa na Wajapani walipoikalia Uchina kuanzia mwaka 1931 hadi 1945