Beijing. Maafisa wawaondoa wakaazi baada ya milipuko.
14 Novemba 2005Matangazo
Maafisa nchini China wamewaondoa wakaazi karibu 10,000 karibu na mji wa Jilin kaskazini magharibi ya China , baada ya milipuko kadha mikubwa katika kiwanda cha kemikali.
Milipuko hiyo siku ya Jumapili mchana iliharibu madirisha mita kadha kutoka mahali ilipotokea na kutoa moshi mkubwa hewani.
Watu walioshuhudia katika kiwanda hicho wanasema kuwa kiasi watu 70 wamejeruhiwa , lakini hakuna kifo kilichoripotiwa.
Bado haijafahamika kilichosababisha milipuko hiyo.
Afisa wa mji huo amesema kuwa uchunguzi unaendelea.