BEIJING. Kiongozi wa upinzani wa Taiwan ziarani China.
29 Aprili 2005Matangazo
Kiongozi wa upinzani wa Taiwan Lien Chan ameitaka China kufungua milango ya mazungumzo na mabadiliko ya kisiasa bila kubadili hali ilivyo baina ya pande zote mbili.
Aliyasema hayo alipohutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Peking katika ziara yake yenye azma ya kuleta uhusiano mwema baina ya China na Taiwan.
Lien ndie kiongozi wa kwanza kutoka chama cha Kuomintang kukanyaga udongo wa China tangu vita vya mwaka 1949 vilipomalizika.
Chama cha KMT kinapendelea muungano na China.
Katika ziara yake anatarajiwa kukutana na kiongozi wa chama cha kikomunisti wa China Hu Jianto baadae leo.