BEIJING: Kimbunga kimevuma mashariki mwa China
12 Septemba 2005Matangazo
Zaidi ya watu milioni moja wamehamishwa kutoka jimbo la mashariki la Zhejiang nchini Uchina kwa sababu ya kimbunga cha Khanun.Upepo mkali na mvua kubwa zilizonyesha kufuatia kimbunga Khanun zimesababisha mafuriko na mmomonyoko wa ardhi katika miji mingi ya jimbo la Zhejiang.Vile vile sehemu nyingi hazina umeme.Safari za ndege pia zimefutwa au zimeahirishwa.Mwanzoni mwa mwezi huu kimbunga kingine,Talim,kiliuwa dazeni kadhaa ya watu,mashariki mwa Uchina baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.