BEIJING: Jawabu la Iran litachunguzwa kwa makini
23 Agosti 2006Matangazo
China inataka kulichunguza kwa makini jawabu lililotolewa na Iran kuhusika na mgogoro wa kinuklia kati ya Irana na nchi za magharibi.Taarifa ya wizara ya kigeni imesema,ni matumaini yake kuwa Iran imetia maanani shaka za jumuiya kimataifa na kama ipasavyo imechukua hatua inayohitajiwa.Siku ya Jumanne,China kwa mara nyingine tena iliyaarifu madola matano yenye kura ya veto katika Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa haiungi mkono kuiwekea vikwazo Iran.Nchi hizo tano na Ujerumani zimependekeza vivutio vya kiuchumi na kisiasa ikiwa Iran itasitisha mradi wake wa kurutubisha uranium.Haijulikani kama Iran katika jawabu lililotolewa,imekubaliana na vivutio hivyo.