BEIJING: Idadi ya vifo yaongezeka
7 Agosti 2006Matangazo
Idadi ya vifo vilivyosababishwa na kimbunga Prapiroon nchini China imeongezeka na kufikia 77, huku watu wawili wakiwa hawajulikani waliko.
Shirika la habari la Xhinhua limeripoti kwamba vifo hivyo vimetokea katika mkoa wa Guangdong, ambako kimbunga Prapiroon, kilipiga Alhamisi wiki iliyopita, na pia katika eneo la Guangxi.
Vifo vingi vilisababishwa na maporomoko ya ardhi, mafuriko na upepo mkali uliosababishwa na kimbunga hicho.