BEIJING Gharika yatarajiwa kuendelea nchini China
6 Juni 2005Matangazo
Watabiri wa hali ya hewa nchini China wameonya kwamba mvua kubwa na mafuriko yataendelea nchini humo. Mvua ambayo imekuwa ikinyesha kwa muda wa juma moja mfululizo imepelekea kuuwawa kwa watu wasiopungua 204 na kuwajeruhi wengine 79.
Gharika hiyo imeathiri raia zaidi ya milioni 17 katika maeneo mbalimbali nchini kote. Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika maeneo yanayopakana na mto wa Yangtse katika kipindi cha siku kumi zijazo na hivyo kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.