Beijing: Familia za wapigania haki za binaadam waliofungwa katika ...
3 Desemba 2003Matangazo
jamhuri ya umma wa China zimemtaka kansela Gerhard Schröder aingilie kati ili waachiliwe huru.Baada ya kukamatwa wanaharakati wawili wa kikristo na adhabu kali jela kupewa wapigania mageuzi ya kijamii,familia za waapigania haki za binadam zimemuomba kansela Gerhard Schröder alizushe suala hilo wakati wa mazungumzo yake pamoja na viongozi wa jamhuri ya umma wa China.Waziri wa sheria wa serikali kuu ya ujerumani,anaefuatana na kansela ziarani nchini China,bibi Brigitte ZYPRIES amekua na mazungumzo hii leo pamoja na waziri mwenzake ZHANG FUSEN na madhamana wa ngazi ya juu wa idara ya sheria mjini Beijing.