BEIJING : China yatathmini maafa ya kimbunga
12 Agosti 2006Wafanyakazi kusini mwa China wamekuwa wakisomba mrundiko wa matope na vifusi mitaani wakati serikali ikitathmini hasara hapo jana kufuatia kimbunga kikali kabisa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 50 nchini humo na kuuwa watu 104 na wengine 190 wahajulikani walipo.
Kimbunga Saomai kimepiga majimbo ya Zhejiang na Fujian hapo Alhamisi na kulazimisha kuhamishwa kwa watu milioni moja na laki saba na kimeharibu maelfu ya nyumba.
Kimbunga hicho kikubwa kimepoteza baadhi ya nguvu zake lakini televisheni ya taifa imemkariri afisa mwandamizi wa serikali akionya watu wasibweteke kutokana na mvua kubwa na pepo kali zinazotabiriwa mwishoni mwa juma.
Hali ya hewa hiyo ya mvua na upepo inazidisha hatari za kuzuka kwa maporomoko zaidi ya ardhi na mafuriko.