BEIJING China yasitiri maiti za wachimba migodi wake.
18 Februari 2005Matangazo
China imeanza kuzisitiri maiti za wachimba migodi 212 waliouwawa kwenye mgodi wa makaa ya mawe Jumatatu iliyopita. Ajali hiyo iliyotokea huko Sunjiawan katika mkoa wa kazkazini mashariki wa Liaoning, umezusha lawama za ukosefu wa usalama wa kutosha kwenye migodi ya China. Gazeti la China Daily, linataka malipo ya fidia kwa jamii za waathiriwa yaongezwe kwa kiwango kikubwa ili kuwashurutisha wenye migodi kuchukua hatua za kuboresha usalama kwenye migodi hiyo. Katika ripoti nyengine iliyotolewa na shirika la habari la Xinhua, idadi ya vifo kufuatia ajali iliyotokea katika mgodi mkoani Yunnan imepindukia 27.