Beijing. China yabana uhuru wa habari.
11 Septemba 2006Matangazo
China imeanzisha sheria mpya ambazo zitafanya kuwa vigumu kwa vyombo vya habari vya nje kufanyakazi katika nchi hiyo. Vyombo vya habari vya nje vitahitajika kupata ruhsa kutoka kwa shirika la habari linaloendeshwa na serikali la Xinhua ili kuweza kusambaza habari na picha.
Sheria hizo mpya pia zinaliruhusu shirika la habari la Xinhua kuchuja habari ambazo zitaonekana kuathiri maslahi ya China.
Vyombo vya habari vya kigeni pia vinaweza kuondolewa liseni yake iwapo vitavunja sheria hizo.
Umoja wa Ulaya umedai kupatiwa taarifa zaidi juu ya sheria hizo.