BEIJING: China imeongeza kiwango chake cha ushuru kwa bidhaa za nguo
20 Mei 2005Matangazo
China imetangaza mipango yake ya kuongeza kiwango cha ushuru wa forodha hadi asilimia 400 kwa bidhaa zake za nguo.
Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya fedha nchini humo, kiwango hicho cha ushuru kitaanza kutozwa mwezi wa juni. Serikali ya China imekuwa chini ya shinikizo za kimataifa za kuitaka ipunguze mauzo yake ya nje ya bidhaa hizo.
Umoja wa Ulaya umetishia kuiwekea vikwazo china ili nchi za ulaya zisiazige bidhaa za nguo kutoka China iwapo nchi hiyo haitatatua tatizo hilo.