Basel: Mchezaji wa kike wa timu ya taifa ya Ujerumani Birgit Prinz na nyota ...
16 Desemba 2003Matangazo
ya timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane wamechaguliwa kua wachezaji bora wa kabumbu kwa mwaka huu.Uamuzi huo umepitishwa na matrena wa timu za taifa chini ya usimamizi wa shirika la kimataifa la kabumbu FIFA.Bingwa wa dunia upande wa wanawake,mwanasoka wa kijerumani Birgit Prinz amewashinda Mia Hamm wa Marekani na Hanna LJUNGBERG wa Sweeden.Hii ni mara ya tatu kwa Zinedine Zidane kuchaguliwa kua mwanasoka bora wa dunia.Nafasi ya pili amechaguliwa mwanasoka mwengine wa Ufaransa Thierry Henry na nafasi ya tatu kushikiliwa na Ronaldo wa kutoka Brazil.