Barcelona yarudi nyumbani na kombe la Ulaya
19 Mei 2006
Kati ya wiki hii,FC Barcelona iliwasili nyumbani kutoka Paris na Kombe la klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuipiga kumbo Arsenal London kwa mabao 2:1.Umati mkubwa wa mashabiki ulijipanga majiani huku timu yao ikipita ndani ya basi na ikishangiriwa kwa kutwaa tena taji tangu mara mwisho 1992.
Mabingwa hawa wa Ligi ya Spain, walikumbana na zahama kubwa ya Arsenal iliocheza na wachezaji 10 tu kabla kuondoka na ushindi.
Baada ya shangwe na sherehe hizo, baraza la mji wa Barcelona, liliarifu vasara ya hadi Euro laki 1 ilifanyika kwa maduka,vituo vya simu n a taa za trafili mariani.
Mashabiki 45 walitiwa kizuizini na wengine 100 walijeruhiwa-hiyo ndio hesabu ya mwisho ya ushindi wa FC Barcelona wa Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Na jioni hii,stadi wa FC barcelona alietia bao la kwanza la kusawazisha juzi katika finali na Arsenal,mkameroun Samuel Eto’o ataibuka mtiaji mabao mengi katika La Liga msimu huu akiuona leo tena wavu katika mpambano na Athletic Bilbao.Eto’o ametia mabao 25 sawa na mshambulizi wa Valencia David Villa na hivyo anahitaji bao 1 zaidi leo kumpiku mwenzake.
Mpambano wa leo hatahivyo, hauna umuhimu sana kwa timu zote mbili ,kwavile, Barcelona wameshatwa ubingwa waq Spain na Bilbao iko nafasi ya 13. Hivyo, haiko hatarini kuteremka daraja ya pili ya ligi ya Spian.
Bundesliga ikiwa nayo imemaliza msimu kwa kuitawaza Bayern Munich mabingwa,imeshaachwa mkono na stadi wake Michael ballaci aliejiunga na Chelsea ya Uingereza.
Taarifa za hivi punde zinasema, stadi wake mwengine-mbrazil Ze Roberto, hana hamu ya kurefusha mkataba; na mazungumzo ya mkataba mpya na Munich hayakuzaa matunda mema.Munich imesema haijui wapi Ze atahamia mara mkataba wake ukimalizika Juni 30.Ze amechaguliwa katika kikosi cha Brazil kwa Kombe lijalo la dunia.
Kwa jumla, Ze Robert atakuwa mchezaji wa 4 kuiachamkono klabu bingwa ya Ujerumani mwishoni mwa msimu huu.Wengine mbali na yeye na ballaci ni Lizzarazu beki wa Ufaransa na Jens Jeremies ambao wanastaafu katika dimba.
Kombe la dunia likinyemelea na zikisalia siku 20 tu kabla firimbi kulia,mfalme Pele amesema wiki hii kuwa, mbinyo juu ya timu ya Brazil kuwa itashinda tena kombe la dunia, utaifanya ipate taabu sana kutimiza shabaha hiyo.Shinikizo,matarajio na bahati mbaya ni mambo yalioziendea kombo timu nyingi zilizopigiwa upatu miaka ya nyuma zingeibuka mabingwa-alionya Pele.
Leo hii, aliongeza, adui mkubwa wa Brazil ni kuambiwa ndio itakayoibuka mabingwa wa dunia.
Pele akiwa sasa na umri wa miaka 65 na mshindi wa vikombe 3 vya dunia,alitoja orodha ya timu kadhaa zilizopigiwa upatu na kuhanikiza zingeibuka mabingwa wa dunia:Pele,aliitaja timu stadi ya Brazil katika Kombe la dunia 1982 huko Spain,timu ya Holland 1974 Ujerumani na 1978 huko Argentina.Ukikumbuka Kombe lililopita la dunia, Pele, alisema Itali na Ufaransa ndizo zilizokuwa timu kali zilizotumainiwa kuwika huko Korea na Japan spande wa timu za Ulaya na Argentina kutoka America Kusini na hakuna hata moja iliopindukia duru ya kwanza.
Kuna nchi 2 kuu ambako dimba halina ushabiki mkubwa:Marekani na India, lakini likiwadia Kombe la dunia,mambo hubadilika.Mare cricket.Juni hii, kote kuwili mfalme dimba atatawala.
Mechi zote 64 zitaoneshwa moja kwa moja nchini Marekani,kwani huko dimba linatia fedha kutokana na mashabiki wa asili ya Spiana u dilatino.Mwaka uliopita vituo vya TV vya ABC na ESPN vilitangaza kwamba vimenunua pia haki za kuonesha makom bey a dunia ya mwaka 2010 huko Africa Kusini na 2014.
Ama nchini India,kila miaka 4 Kombe la dunia likipiga hodi,India huweka kando mchezo wake maarufu wa cricket ili kuangalia dimba.Idadi ya walioangalia kombe la dunia lililopita huko Krea ya Kusini na Japan, ilipindukia ile ya mashabiki wa dola za kabumbu,Brazil,Uingereza na Argentina licha ya kuwa India, haikuwahi kucheza katika kombe la dunia.Mechi zote huko zitaooneshwa moja kwa moja .