Barcelona, Bayern na Inter zasonga mbele Champions
12 Machi 2025Matangazo
Barcelona, ilifanikiwa kuipiku Benfica kwa ushindi wa mabao 3-1 na sasa ikitarajiwa kukutana na Borussia Dortmund ama Lille kwenye robo fainali.
Bayern Munich nayo iliiondoa Bayer Leverkusen, zote za Ujerumani kwa jumla ya mabao 5-0 huku Inter Milan nayo ikitinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Fayenoord kwa mabao 2-1.
Liverpool vinara wa ligi ya Premier nayo imetupwa nje ya michuano hiyo ya Champions kwa jumla ya mabao 4-1 dhidi ya PSG ya Ufaransa.