MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Baraza la Usalama la UN laitaka Rwanda kuacha kuwasaidia M23
22 Februari 2025Matangazo
Linatoa wito huo wakati waasi hao wakizidi kusonga mbele katika maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo.
Azimio hilo la Ijumaa lililopitishwa kwa kauli moja la Baraza la Usalama linalaani vikali mashambulizi na hatua zinazopigwa naM23 huko Kivu Kaskazini na Kusini kwa kushirikiana na Vikosi vya Ulinzi vya Rwanda.
Aidha, linatoa wito kwa Vikosi hivyo vya Rwanda kuacha kuwasaidia waasi hao na kuondoka mara moja nchini Kongo bila masharti.
Awali Baraza hilo liliitoa wito wa "kusitishwa kwa mapigano mara moja. bila masharti", lakini jana Ijumaa nchi zote zikiwemo nchi tatu za Afrika zilinyooshea kidole Kigali.