Baraza la Usalama la UN kuchukuwa hatua kali dhidi ya Kongo
2 Aprili 2025Bonnafont amesema hayo kwa vyombo vya habari wakati nchi yake inachukuwa uongozi wa baraza hilo kwa mwezi huu wa Aprili.
Waasi wa M23 waendelea kukamata miji muhimu ya Kongo
Bonnafont amesema siku chache zilizopita, walipata maelezo kutoka kwa mjumbe maalumu wa Umoja huo nchini Kongoaliyewaeleza kuhusu hali ilivyo na kwamba mjumbe huyo alisema kundi la M23 linaendelea kusonga mbele kwa msaada wa vikosi vya Rwanda.
Baraza la Usalama la UN lataja dharura ya kusitisha vita Kongo
Bonnafont, pia amesema Baraza hilo la Usalama lilitaja haja ya dharura ya kusitisha mapigano wakati kundi hilo la M23 limechukuwa udhibiti wa maeneo makubwa ya majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini nchiniKongo huku njaa na mapigano yakisababisha watu wengi kupoteza makazi yao.