Baraza la haki za binadamu la UN kukutana kuijadili Congo
4 Februari 2025Matangazo
Msemaji wa Baraza hilo Pascal Sim amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba, kikao hicho kitakachofanyika Ijumaa jioni kitajikita kwenye hali ya haki za binaadamu kwenye eneo hilo.
Kongo iliomba kikao hicho cha dharura hasa baada ya waasi wa M23 kuukamata mji wa kimkakati wa Goma. Utulivu umerejea Goma, baada ya muungano wa waasi kutangaza kusitisha mapigano ili kupisha huduma za kiutu.
Rais Cyril Ramaphosa aapa kutoitupa mkono Kongo
Wakati huo huo, Waziri wa Mawasiliano wa Kongo Patrick Muyaya alisema jana usiku kwamba zaidi ya miili 2,000 ya watu waliouawa kwenye mapigano inasubiri kuzikwa.