Baquba, Iraq: Vikosi vya Marekani vyashambulia vito Iraq Vikosi vya ...
19 Novemba 2003Matangazo
Marekani jana vilitumia mabomu, mota na mizinga, vikijaribu kukomesha upinzani wa wapiganaji wa chini kwa chini nchini Iraq, huku Rais George W.Bush na waziri wake wa mambo ya nje Colin Powell wakijitafutia msaada barani Ulaya kuhusu kampeni yao iliyoingia matatani. Kikosi cha nne cha jeshi la Marekani kilisema ndege za F-15 na F-16 zilibwaga mabomu 12 ya tani 500, katika mashambulizi makubwa kabisa saa za usiku kaskazini mwa Iraq, tangu vilipomalizika rasmi vita tarehe Mosi Mei. Mashambulizi hayo yalikuwa sehemu ya operesheni ya vikosi vya Marekani mwezi huu nchini humo, vikijibu hujuma dhidi yao, ambazo ziliwaua Wamarekani 177 kwa uchache mnamo kipindi cha zaidi ya miezi sita.