BALUCHISTAN : Kiongozi mashuhuri wa waasi auawa nchini Pakistan
27 Agosti 2006Matangazo
Pakistan imeataaruifu kuwa kiongozi mashuhuri wa waasi Nawab Akbar Bugti ameuawa katika jimbo la Baluchistan kusini magharibi mwa Pakistan.
Kiongozi huyo aliuawa katika mapigano baina ya majeshi ya serikali na waasi katika jimbo hilo .
Askari 20 wa serikali waliuawa katika mapambano hayo.
Kiongozi huyo Akbar Bugti aliekuwa na umri wa miaka zaidi ya themanini alikuwa anaendesha kampeni ya kupigania kujitawala kwa jimbo la Baluchistan na kudhibiti sehemu ya mapato yanayotokana na mauzo ya gesi.
Waziri wa habari wa Pakistan amethibitisha kifo cha kiongozi huyo wa waasi.